Kama kawa katika kupata burudani na mengine mengi, sasa ili kuhakikisha
zoezi linaenda sawa lazima computer yako iwe na uwezo wa kupiga mziki,
iwe inashika wireless networks uweze download nyimbo za mbali mbali, Pia
Graphics ni muhimu sana ziwe vizuri, na vingine vingi, leo Ningependa
kushare nawe somo la drivers kwa computer, unajua drivers ni nini?? kazi
zake, drivers muhimu ni zipi, sehemu ipi ya computer unaweza pata
drivers, na jinsi ya kuinstall drivers zako.....Karibu.
Drivers ni software part katika computer system ambayo kazi kubwa ni ku
LINK kati ya Operating system softwares na Hardwares ambazo zinakuwepo
ndani ya computer yako, Drivers huusika katika kuleta uelewano wa hizi
system mbili za computer.....
Labda nkupe mfano mzuri, wewe computer yako haina BUILT in Bluetooth
Card ambayo yenyewe ni Hardware, then unataka kuinstall bluetooth
software driver kwa computer yako, unajua nini hutokea, kuna either
kugoma kuinstall, ama ikainstall alafu ukawa unapata BLUESCREEN problem kwenye computer yako.
Kuna njia nyingi sana za kuinstall drivers kwa computer yako, hutegemea
na uwezo wa computer yako katika njia moja ama nyingine, ...Leo complex
system tunakupa njia zote muhimu za kuinstall drivers zako kwa computer
yako ili mambo mengine yaende sawa.
NJIA NI KAMA HIZI
Click Start nenda kwa My computer Tab alafu Right Clik kisha bonyeza Properties, ikifunguka enda kwa device manager TAB iko upande wa kushoto juu....then click ....kama inavyoonekana hapa
Ikitokea kwenye computer yako zinaonekana hivi, maana yake drivers zote
zipo, lakini ikitokea ina Onekana tofauti labda inaleta Rangi Ya njano
ivi...Jua hapo driver imemiss....sasa kuna computer zingine drivers zote
zipo ila bado unakuta haipigi mziki, hii inakuwa labda drivers are
outdated, ama zimejificha kwa processor yenyewe.....Ushawahi kutana na
tatizo hili, twende sawa tutatue wote.
kwa Mfano Unamiss Sound drivers, nenda kwa Sound, Video and Game Controller, then angalia ile driver inayomiss, then i right CLICK alafu baada ya hapo click update itafunguka kama hivi,
Baada ya hapo unakuja katika uchaguzi, u update online ama on a
computer, ukitumia online ni moja kwa moja uwe connected na
internet...lakini ukibrowse from computer nako kuna njia zake kama
inavyoonekana hapa, na kwa njia hii driver yako inakuwa updated fresh.
Ukitaka kucheki kwa computer kuna vitu viwili vya kuzingatia,
NJIA YA KWANZA
Kama una Universal Drivers package ambayo hukuwezesha kusearch for drivers in all folders....kama inavyoonekana hapa
NJIA YA PILI
Hii njia huusisha utaftaji wa drivers za computer yako ndani ya
processor, or system nzima ya computer kokote, kuna wakati Operating
System yako huingia na baadhi ya drivers lakini huweza kutofanya kazi,
hata ukiweka drivers zote unaweza kuta vitu vingne havifanyi kazi kama
vile sound haipigi na drivers umeweka, wireless hakuna na ushainstall
drivers...hii sasa ni kiboko yake, pale pale kwenye device manager na
update driver....kama inavyoonekana hapa
Na hapa ndo tunakoenda kwa system driver yenyewe automatically huleta
hii kitu, yaani huspecify driver unayotafta ....kumbuka hapa tulikuwa
yunacheki Sound Drivers kama mfano wetu....kama inavyoonekana driver
yake..kilichobaki ni kubonyeza NEXT kwisha habari yake.
NOTE: Njia ya pili ni kwa ajili ya pindi unapokuwa umeweka drivers zote lakini bado computer yako drivers kama hazifanyi kazi hivi
NJIA NYINGINE RAHISI ZAIDI NI IPI???
Hapa sasa tunatumia software mbali mbali kwa computer yako, complex system tunarecommend utumie, COBRA DRIVER PACK SOLUTION ama DRIVER PACK SOLUTION 2013/14
download hapo kwa hiyo link kama unaUtorrents ama bittorrents tayari
kwa computer yako.....ni rahisi zaidi, lakini hu shindwa wakati
mwingine.
NJIA YA MWISHO KABISA
Najua wengi hatupendi umiza kichwa kwa mambo za drivers, lakini leo pia
complex system tumeona sio mbaya kukupa njia za kuinstall drivers za
computer yako kwa urahisi zaidi.
Click Start kwenye computer yako then type "windows update" alafu ENTER baada ya hapo check for updates, ikimaliza install automatically, hii huitaji uwezo wa internet yenye kasi kidogo.
NOTE: KAMA WINDOWS YAKO SIO GENUINE WINDOWS FROM MICROSOFT, U
WILL NOT SURVIVE FOR LONG TIME WINDOWS ITALETA KELELE ZA WINDOWS IS NOT
GENUINE, COZ NJIA HII NI KWA AJILI PIA YA WINDOWS VALIDATION.
.......Tunaamini tuko sawa juu ya hili, sasa unapopata shida kokote
karibu post tuwekane sawa....na pia usisahau ku share hizi habari kwa
friends wa FB na magroup yoyote kwa FB, na kokote pale twitter, yahoo,
youtube, hotmail, msn na kwngneko.....Karibuni Sana
Jinsi ya kuweka wireless driver...msaada
ReplyDelete