Thursday, 25 September 2014

COMPUTER HARDWARE

Any fool can write code that a computer can understand. Good programmers write code that humans can understand.
Last Edit: 2 weeks 3 days ago by Man Pierre. Report to moderator

FAIDA NA HASARA ZA KU UPDATE BIOS: 2 weeks 3 days ago #2988

  • Man Pierre
  • Man Pierre's Avatar
  • OFFLINE
  • Administrator
  • Posts: 621
  • Thank you received: 290
Kama usemavyo BIOS ndio BASIC Input Output System, Ndio system pekee inayoweza ifanya computer iwake ikiwa inajua kitu gani kipo, kitu gani kinatatizo, na huwa inatoa information kwa kile ambacho inakiona hakiko sawa.

BIOS ni ile system ambayo inakagua computer kabla ya kuwaka na kuanza kufanya kazi, BIOS ndio inaangalia RAM ipo, HDD ipo, Kuna Flash ama CD kwa ROM/PORTS. Ndio ile system ambayo tunaweza iita READ ONLY MEMORY PEKEE ambayo inaweza kutunza taarifa chache sana.



KWANI KU-UPDATE BIOS NDO KUFANYAJE? NDO KUNA KUAJE KUAJE, SABABU? ULAZIMA??

Ni Maswali ambayo huweza kujiuliza wakati ukisikia watu wanataka update BIOS. BIOS ni kile ki(FIRMWARE) kilichotengenezwa kwa ajili ya kutambua kila kitu ndani na nje kwa maana ya OUTPUT DEVICES kwa computer.

Kina uwezo wa kujua drivers zote ziko sawa, kina uwezo wa kutambua Network Interface Card ipo ila haijawa plugged in fresh, inaweza jua kuwa kuna FAN lakini computer bado inachemka (Overheating).

Ina uwezo wa kutambua kuwa kuna kuna POWER FAILURE kwa namna yoyote ile iwe Charger haiingizi Moto unaotakiwa, ama battery life iko LIMITED.



Unaweza sema si sawa kama umetazama wakati Computer ina operate, Hapa nazungumzia BIOS wakati unapowasha tu mashine ama maandalizi ya kuwasha computer yako na ikaanza kuwaka.

KU-UPDATE BIOS

ku-UPDATE BIOS maana yake ni kufanya mabadiliko ya baadhi ya functionalities za BIOS na CHIP zake. Yawezekana ku-update BIOS ukafanya kwa njia tofauti tofauti kutegemeana na BIOS yako.

Unaweza update BIOS kwa kubadili BIOS CHIP, Hii sasa Hutegemeana na kama BIOS Chip zako ziko MOUNTED kwa Motherboard moja kwa moja na manufacturer. Ukibadili BIOS chip basi hakikisha unachukua ile yenye uwezo wa kuendana na uwezo wa motherboard yako.


Unaweza ku-update BIOS kwa Kutumia BIOS UPDATE TOOLS hizi tools mara nyingi huwa zinatolewa na Manufacturers. So hakikisha unajua manufacturer wako ni nani? na website yake kwa ajili ya kupata updates kwa ajili ya aina ya Computer yako.

NAMJUAJE MANUFACTURER WANGU na AINA YA BIOS YANGU

Unaweza mjua manufacturer mara nyingi huweza andikwa kwa BIOS yenyewe, ama hata kwa User Manual ya Motherboard ya computer yako, hii inategemeana kwa wale wanaonunua computers kutoka kwa manufacturers huweza pata. ila kwa wewe tazama hapa

Fungua msinfo32 kwenye search box ndani ya computer yako alafu utaona BIOS yako kama hivi


Bios.jpg


Baada ya kugundua hayo basi zoezi la kutafuta update kwa BIOS yako linaweza endelea.


TARATIBU ZA KU-UPDATE

Wakati ukitaka ku-update BIOS tafadhali HAKIKISHA UMEJIKAMILISHA KWA HIVI VITU:

1. Hakikisha unapata UPDATE SOFTWARE ya BIOS Moja kwa Moja toka kwa Manufacturer wako




2. Hakikisha ukitaka ku-update una UHAKIKA WA CHARGE kwa computer yako (POWER)

3. Hakikisha Process ya ku-update haiwi interrupted by ANY PROGRAM

4. Hakikisha unajua unachokifanya, Hii Process huweza ifanya computer iFLASH wakati wote wa ku update na zingine huweza kuzima kabisa moja kwa moja kama tu inachukua kitu chenye uwezo zaidi na motherboard.

5. Hakikisha umefanya BACKUP ya BIOS FIRMWARE iliyopo ili incase mambo ya yamekwenda visivyo urudie backp iliyopo




LENGO LA KU-UPDATE BIOS LA MSINGI KABISA LINAPASWA KUWA LIPI???

Lengo kubwa la BIOS Update kwa computer yako, Nashauri liwe Ndani ya haya:

1. Umebadili baadhi ya components za computer yako na computer inashindwa kufanya kazi vizuri, mfano Processor, CMOS Battery, Mounted Ports and Chips

2. Umeongeza Computer Drivers na Baadhi ya hardware parts mfano Sound Card, Video Card, Controller, Bus Controller, Network Chips and ROM Chips

3. Endapo Computer yako ina tatizo la BIOS labda mfano ime CORRUPT, ama iko OUTDATED na Manufacturers wakati unanunua walishauri u-update BIOS yako.


FAIDA ZA Ku-UPDATE BIOS NI ZIPI ???

Kwanza hufanya computer kuwa na uwezo wa kuwaka kirahisi na kuifanya computer iweze kitambua components zake kirahisi zaidi, (japo wepesi wa computer hutegemeana na RAM, Processor na other factors-virus, overheating etc.

Pili computer kuweza kutambua any INPUT/OUTPUT Devices kwa haraka zaidi, yaani huwezesha computer Operating System kuweza kutambua kwa haraka devices zinazokuwa inserted. Hii Pia husaidia katika drivers instalations kwa baadhi ya devices mfano Printer, Projectors, Other Devices E.g Camera


HASARA ZA KU-UPDATE

Napenda fananisha BIOS na Kati Kati ua Usingizi MZITO na KUAMKA (pale kati kati sasa panapounganisha). Ku update BIOS kunaweza ifanya computer yako ishindwe wakati mwngine kutambua hata vitu vidogo kabisa kama USB PENDRIVE(Flash)

Ikitokea tatizo lolote wakti wa ku-update BIOS yaweza kufanya BIOS yako kuCORRUPT na hvyo kukulazimu kushindwa kuitumia computer yako vizuri.

Pia Inaweza ikasababisha tatizo la KUHARIBIKA kwa baadhi ya CHIPS ambazo ziko related na BIOS, hivyo unatakiwa uchukue tahadhari hiyo.


USHAURI

USI-UPDATE BIOS ya computer kama majaribio ya kisayansi wakati ndo computer hiyo hiyo inayokuwezesha kuingia complex system na kupeana mawili matatu na wadau.

kama hujui kitu juu ya ku-update BIOS peleka computer kwa mtaalamu wa mambo ya BIOS sio kwa mtu anayeweza kufanya installations za windows 7

Ni hayo ambayo ningependa SHARE nanyi wadau, kama una cha kuongezea itakuwa POUWA...Kama imekusaidia THANKYU :dry: :dry: :whistle: :whistle: :whistle: :whistle: :whistle:

1 comment:

  1. Thank you for this article. It's really helpful for us. Virtual Voyage College, Indore is one of the best colleges in India. Hardware & Networking Courses in India

    ReplyDelete