Siku za hivi karibuni nilishare somo lililokuwa likihusu Microsoft .NET Framework
Rafki yangu mmoja akaona si mbaya akiniuliza inbox namna gani angeweza
kujua ni version gani ya .NET Framework imekuwa installed kwenye system
yake.
Katika kufanya tafiti za hapa na Pale nikagundua Njia mbili zinazoweza
kuku wezesha kugundua ni aina gani ya .NET Framework iko installed kwa
OS yako.
Njia ya Kwanza ni kwa kutumia Registry
1. Andika "regedit" pale kwenye RUN au click Start Menu Search box halafu bonyeza Enter. Itafungua Registry
2. sasa nenda step kwa step kwa location hii hapa :
HKEY_LOCAL_MACHINE\SOFTWARE\Microsoft\NET Framework Setup\NDP
3. ukishafika hapa utaona version tofauti tofauti zilikuwa installed tayari katika OS yako
Njia yaPili ni kwa kutumia Windows Explorer
Microsoft .NET Framework zoote zinakuwa installed kwenye directory hii hapa
%windir%\Microsoft.NET\Framework\
Kwahyo copy hiyo path kisha i paste pale kwenye dialogue box kisha
bonyeza Enter itafungua folder kama ulionalo hapa kwa screen shot
Hivyo kwa kupitia Folder hilo utaweza tambua ni Version ipi ya .NET Framework imekuwa installed
Mi nimegundua hizo kama kuna zingine wadau tujuzane kwa comments hapa chin
No comments:
Post a Comment