MICHAEL JOSEPH KWAYU=0763-690-270
Bwana Yesu apewe sifa.
Leo nitaongelea huduma ya uimbaji kanisani.
Nimekuwa katika huduma mbalimbali kwa muda mrefu katika kanisa.
Lakini nimefika mahali nikachaguliwa katika huduma ya kusimamia uimbaji au kuongoza kwaya katika kanisa,hii ndio huduma ambayo inavikwazo vingi sana. Nimegundua kwanini shetani alishindwa mahali hapa kwani kuongoza kundi lisilohitaji kuomba wala kujua neno bali ni kuimba na kutoka au kuimba ndio mwisho ni ngumu sana,wanakwaya wengi au waimbaji wanachofahamu katika kanisa ni kuimba tu wakiimba wako rohoni sana wakimaliza kila jambo wameliacha madhabahuni huku kwingine ni mwili unatenda kazi.
Kwanza huwezi amini kwenye kanisa moja chini ya mchungaji moja kanisa moja bali kwaya kuu na kwaya ndogo hazina mahusiano kabisa zinashindana hazipendani majungu na fitina kama mataifa hiyo ni shida katika kanisa upendo wa kristo katika kwaya haupo kabisa.
Naona kama hivyo ndio huduma basi watakuwa wa kwanza kuhukumiwa maana Mungu anasema mlitumika bali siwatambui itakuwa ni kilio siku ile tena kikuu sana kwa waimbaji,fedha imekuwa ndio miungu yao pamoja na walimu wa kwaya maana kama wengine wanapeleka fedha katika makanisa na huduma mbalimbali waimbaji wanataka fedha kutoka kwa kanisa na washirika ili wafanye mambo yao hii sio injili ya Yesu bali ni ya adui shetani.
Ifike mahali kanisa lipone na liwe kitu kimoja katika huduma zote zinazofanyika kanisani kama nigepewa jukumu la kuchagua basi nisingekubali huduma za uimbaji wa namna hiyo katika makanisa ni bora kuwa na kundi la sifa kuliko kuwa na kwaya zenye mizozo na fitina kanisani,maana hapo hakuna Mungu tena bali shetani anashika nafasi katika kundi hili.
Hili ndio kundi linalorudisha nyuma huduma nyingi sana na ndio kundi linalopewa kipaumbele katika kila jambo kanisani kabla ya huduma yoyote huitwa na kuimba na kusifu ndipo huduma zingine hufuata bali limeingiliwa na adui mbaya kabisa shetani tena ni Yule joka kuu maana anataka kuangamiza kanisa la sasa,Ndugu zangu katika kristo Yesu nilikuwa namsikiliza mchungaji Abiudi akisema kuhusu huduma hii niliona ni kawaida tu lakini baada ya kuingia nimeijua vizuri na nimewagundua hawa waimbaji ndio chanzo kikuu cha kanisa la Mungu kuharibika maana hawafuati kabisa kanuni za Yesu kristo katika huduma hii.
Hivyo kanisa la leo linamzigo mzito sana wa kuomba kwa ajili ya huduma hii ya uimbaji maana ndio chanzo kikuu cha ushirika wa kristo Yesu juu ya kanisa lake na shetani anajua mlango huu maana yeye aliutumikia kabla ya kufukuzwa katika huduma hii hivyo ni vizuri tukaiweka huduma hii ya uimbaji mbele za Bwana kila mara ili kanisa lipate kusonga mbele katika huduma nyingine,nanyi waimbaji ni wakati wenu sasa kurudi katika mstari mnyoofu maana mmekuwa kwazo kwa kanisa kwa ajili ya tabia na mienendo yenu,hata mnafanya kanisa la Mungu kudharauliwa kwa ajili yenu nyinyi ambao mumeandamana na baba yenu iblisi katika kutenda uasi ndani ya kanisa.
Najua kuna watakao kwazwa kwa maneno haya lakini ni bora kukwazwa lakini ukapona kuliko kupotea katika shimo lile la moto wa jehenam maana yeye huja kuu na kuchinja bali kristo alikuja kutafuta aliyepotea ili amrudie Mungu wake apate kuthi ufalme wa mbinguni.
Mungu wa baba yangu Ibrahimu na Yakobo awabariki na muwe na amani ya Kristo mioyoni mwenu.
Ameni.