Wednesday, 29 January 2014

MICHAEL KWAYU.BLOGSPOT.COM.HABARI MPYA

Nape Nauye na AbdulRahman Kinana (Viongozi wa CCM) wanasema kuna
mawaziri mizigo, Lipumba wa CUF anasema “Mawaziri mizigo ni matokeo ya
rais mzigo, na Rais mzigo ni matokeo ya chama mzigo, watanzania tuitue
mizigo yote hii mwaka 2015(Mawaziri mizigo, Rais Mzigo na chama mzigo)",


Maneno hayo hapo juu yamesemwa na Prof. Ibrahim Haruna Lipumba - Mwenyekiti wa CUF Taifa, 26 Januari 2014.

Kuna watu wanaitetea Serikali ya CCM wakati viongozi wa CCM wenyewe wanailipua hadharani, Raisi
wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM amesafiri kwenda nje ya nchi safari ya
358 tangu aingie madarakani mwaka 2005, ametumia miaka miwili akisafiri
kama “VASCO DAGAMA”, Yule mvumbuzi wa kigeni. Mwaka huu wa fedha peke
yake tayari Rais ameshatumia bajeti yote ya safari za nje wakati bado
miezi 6 imebakia ili akamilishe bajeti ya mwaka.
Nakisi ya bajeti ya
Serikali ya Tanzania imetoka shilingi bilioni 389 mwaka 2007 hadi
shilingi bilioni 3000 sawa na trilioni 3 mwaka 2012.

DENI LA
TAIFA limetoka shilingi trilioni 5.9 mwaka 2007 hadi shilingi trilioni
22 mwaka 2012, MKAPA alitumia kipindi chake chote cha uongozi kulipa
madeni yaliyokuwa yameshindikana na JK anatumia kipindi chake chote cha
uongozi kukopa zaidi na kutumia zaidi ili Rais ajaye awe na kazi ya
kulipa madeni miaka 10..... Haya ndiyo matokeo ya MAWAZIRI MIZIGO, RAIS
MZIGO na SERIKALI MZIGO.

Eti mashabiki wa CCM wa kufa na kupona
ambao hamtafakari mnataka kutulazimisha tuamini haya yote yanatokea kwa
bahati mbaya...Nape na Kinana wako sawasawa, na ni viongozi wa CCM,
Lipumba yuko sawa zaidi, yeye anasema tatizo ni kubwa zaidi, siyo tu
mawaziri ni mzigo, bali ni rais na chama chake...Tupingane kwa hoja na
data!